MICHEZO
Wachezaji wa Simba washindwe wao tu sasa hivi hiyo ni baada ya kuhakikishiwa kupewa pesa ya maana katika michezo miwili ya robo fainali ya AFL dhidi ya Al Ahly.
Simba Octoba 20 wanatarajia kukipiga na Al Ahly katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano mipya ya AFL kwenye dimba la Mkapa,Dar.
Kabla ya kuanza michuano hiyo tayari Simba imeweka kibindoni bilioni 1 kama pesa ya maandalizi kwenye michuano inayoshirikisha timu 8.
Taarifa kutoka kwenye uongozi wa Simba hasa kutoka kwenye ofisi ya Rais wa heshima wa klabu hiyo Mohammed Dewji ni kuwa utakuwa bega kwa bega na wachezaji kuhakikisha fungu hilo lililotoka kwaajili ya maandalizi liwe hasa kwa kiasi kikubwa kwa wachezaji kama motisha ya michezo miwili.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Simba, Salim “Try again ” alisema kuwa,
“Tunachokizingatia katika michuano hii ni kwamba tunahitaji kufanya vyema hivyo tumeona katika pesa zile za maandalizi ambazo tumepewa na wasimamizi tunawapatia wachezaji ili wawe na morali nzuri .
“Al Ahly ni timu kubwa lazima sisi tuweze kuwa na mipango sawa katika kila namna ,wachezaji lazima wawe katika hali nzuri ili waweze kufanya kazi yao bila ya kuwa na wasiwasi na tunaamini watafanya vyema”.