MICHEZO
Klabu ya Barcelona ipo kwenye vita kali na Real Madrid kuwania saini ya mchezaji wa Manchester City, Julian Alvarez.
Barca wanalazimika kurejea sokoni baada ya Mshambuliaji wao ,Robert Lewandowski kupata majeraha na kupelekea kutetereka kwa safu yao ya ushambuliaji ,jambo ambalo limefanya kuamua kuelekeza nguvu zao zote kwa Mshambuliaji huyo wa Manchester City, Julian Alvarez.
Mabingwa hao watetezi wa ligi ya La Liga walifanikiwa kuinasa saini ya kinda wa Athletico PR, Vitor Roque kutoka Brazil kabla ya Mshambuliaji huyo kupata jeraha la kifundo cha mguu ,ambapo anatarajiwa kuwa fiti kabla ya kuhamia rasmi Barcelona, mwezi Januari.
Ingawa Vitor Roque anaweza kuwa mchezaji bora katika siku zijazo,klabu hiyo itahitaji mchezaji imara ambaye anaweza kusaidiana na Lewandowski anayeelekea ukingoni.
Mshindi huyo wa kombe la Dunia na Argentina, yuko katika kiwango cha hali ya juu msimu huu baada ya kupachika mabao 6 na kutoa msaada wa goli 5 katika mechi 13 za Manchester City kwenye mashindano yote,Manchester City inashiriki Ligi kuu ya England.
Hata hivyo, sio Barcelona wanaohitaji huduma ya Mshambuliaji huyo pekee mwenye umri wa miaka 23 ,kwani Real Madrid wamepanga kumsajili iwapo watakwama kumsajili Kylian Mbappe msimu ujao.