WAKONGOMANI WALITAKA JESHI LA AFRIKA MASHARIKI KUONDOKA

0:00

HABARI KUU

Muungano wa vyama vya kiraia katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 umefanya maandamano mjini Goma ukitaka kikosi cha pamoja cha Afrika Mashariki kuondoka Mashariki mwa nchi hiyo kutokana na kushindwa kukabiliana na waasi wa M23.

Mwezi Novemba mwaka jana, Kenya 🇰🇪, Burundi 🇧🇮, Uganda 🇺🇬, na South Sudan 🇸🇸 zilituma wanajeshi wake DRC ,chini ya bendera ya jeshi la kikanda la Jumuiya Ya Afrika Mashariki (EACRF) ,kujaribu kulipokonya silaha kundi hilo la waasi na kuleta amani.

M23 imeendeleza kuyashikilia maeneo ya miji na vijiji vya Kivu Kaskazini.

Watu saba waliuawa mapema mwezi huu katika eneo hili. Wiki iliopita,Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Patrick Muyaya aliithibitishia idhaa ya Kiswahili ya BBC kwamba serikali yake haitawapa tena kandarasi wanajeshi wa kikosi hicho cha Jumuiya Ya Afrika Mashariki (EACRF).

Alisema wanajeshi wa Congo watafanya kazi nzuri kuliko EACRF ambao pia amesema wanatakiwa kuondoka mwezi Desemba.

Katika taarifa ya hivi karibuni Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisema vikosi vyake vimejitolea kufanya kazi kwa bidii pamoja na Serikali ya Congo huku likitaja mafanikio makubwa hasa ya kuhakikisha wakimbizi wanarejea salama.

Goma pia imeshuhudia maandamano makubwa dhidi ya ujumbe wa umoja wa Mataifa nchini humo.

Zaidi ya watu milioni 6.2 wamelazimika kuondoka makwao Mashariki mwa nchi hiyo na wanaishi kwingine nchini DRC, na wengine milioni moja na wengine wametafuta hifadhi ndani ya Afrika, hii ni kulingana na takwimu za umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Hosts France will play Argentina in the...
Crystal Palace striker Jean-Philippe Mateta got the opening goal for...
Read more
JKT IPO MBIONI KUACHANA NA MATUMIZI YA...
HABARI KUU
See also  MKUU WA WILAYA ATOA AMRI YA KUWACHAPA VIBOKO WANAOTAKA KUVUNJA MUUNGANO
"JKT TUKO TAYARI KUTEKELEZA, MATUMIZI YA NISHATI SAFI...
Read more
MUHIMBILI-MLOGANZILA YAINGIZA BILIONI 8 KISA UREMBO
HABARI KUU Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema...
Read more
MAMBO 10 YA MSICHANA ANAYEKUPENDA ...
MASTORI Duniani kila mmoja wetu angetamani kuwa na mtu anayeendana...
Read more
MASWALI AMBAYO HAYAJIBIWA KUHUSU GHOROFA LILILOANGUKA KARIAKOO.
Na Askofu, MWAMAKULA Leo, tarehe 21 Novemba 2024 zimetimia siku 6...
Read more

Leave a Reply