NYOTA WETU
Rais Samia Suluhu Hassan ameibuka tishio kwa vyama vya upinzani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa 2025 kutokana na umati mkubwa anaovuta kwenye ziara zake akiwa kwenye mikoa mbalimbali.
Popote aendako kwenye ziara zake kwenye mikoa mbalimbali, Rais Samia amekuwa akilakiwa na umati mkubwa wa watu jambo ambalo sasa ni nyota ya kijani kwake kuelekea Uchaguzi wa 2025 anaweza kuibuka kidedea mapema.
Kada mbalimbali za wananchi,ikiwemo ya vijana madereva bodaboda ,kina mama lishe, wakulima ,wavuvi,wafugaji ,wafanyabiashara na wananchi wa kawaida wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kumlaki Rais ,kitu ambacho akikuwahi kutokea.
Ingawa bado ni mapema mno na Rais Samia bado hajatangaza nia yake ya kugombea urais 2025, lakini ni wazi Rais Samia kwasasa anaonekana ni mwanasiasa mwenye ushawishi zaidi kwasasa nchini na ni turufu kubwa ya uchaguzi mkuu.
Katika ziara zake za hivi karibuni kwenye mikoa ya kusini na katikati mwa nchi amejizolea maelfu ya watu hasa mkoa wa Singida ambayo ilionekana ni ngome ya Lissu lakini imekuwa tofauti kwani amepata watu wengi .