HABARI KUU
Mamlaka ya Uchina inachunguza baada ya video iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha mfanyakazi kutoka Tsingtao akikojoa kwenye tanki ,linaloaminika kuwa na viambato vya bia.
Klipu hiyo iliyotazamwa na mamilioni ya watu kwenye mitandao ya kijamii.
Kampuni hiyo inasema iliwaarifu polisi mara baada ya video hiyo kujulikana, na kuongeza kuwa viungo Katika tanki hilo vilikuwa vimefunikwa.
Tsingtao ni mojawapo ya wazalishaji wakuu wa bia nchini China na muuzaji wa nje mkubwa.
Katika klipu hiyo iliyoonekana mtandaoni siku ya Alhamisi,mfanyakazi, aliyevalia sare na kofia ya chuma ,anaonekana anapanda juu ya ukuta mrefu na kuingia kwenye kontena kabla ya kukojoa ndani yake.
Lebo ya eneo la klipu hiyo inasomeka
“Kiwanda cha bia ya Tsingtao no.3”
Chombo cha habari nchini The paper kiliripoti Ijumaa.
Kituo cha biashara cha ” National Business Daily ” baadaye kilitaja chanzo cha ndani kikisema kuwa aliyechukuwa video hiyo na anayeonekana ndani yake hawakuwa wafanyakazi wa moja kwa moja wa kampuni hiyo.
Katika taarifa iliochapishwa siku ya Ijumaa, ofisi ya usimamizi na utawala wa soko la Pingdu City ,ambako Kiwanda hicho kipo,ilisema walituma timu ya mara moja ya kuchunguza kwenye eneo hilo baada ya kuiona video hiyo ,na kuziba viungo vilivyoonekana kwenye video.
Pia iliongeza kuwa ofisi hiyo itashughulikia suala hilo kwa umakini mara baada ya taarifa kuthibitishwa.