MICHEZO
Inaripotiwa kuwa klabu ya Al-Nassr kutoka ligi kuu ya Saudia Arabia, imedhamiria kumsajili kiungo wa Manchester City, Kelvin De Bruyne.
Tayari klabu hiyo imewasiliana na wakala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ili kukutana na kuelezea mkakati wao wa muda mrefu wa kumshawishi kiungo huyo Mshambuliaji ajiunge nao.
De Bruyne mwenye umri wa miaka 32 amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake wa sasa .
Hata hivyo ,kiungo huyo anasalia kuwa nguzo muhimu ya kikosi cha Pep Guardiola japokuwa amecheza mara moja kwenye msimu huu wa ligi kuu ,kufuatia jeraha la misuli.
Vilevile City wanadaiwa kusitisha mazungumzo ya mkataba mpya na De Bruyne mpaka atakapo pona jeraha lake ,hatua inayochochea zaidi tetesi hizo za kutimkia Saudia Arabia.
Ikiwa dili hilo litakamilika basi, De Bruyne ataungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa City ,Aymeric Laporte pamoja na wapinzani wake wa zamani wa Premier League, Cristiano Ronaldo, Sadio Mane na Alex Telles.