HABARI KUU.
Wazee wa jamii ya Nandi nchini Kenya wametoa wito kwa kurudisha fuvu la Koitalel Arap Samoei ,chifu pamoja na kiongozi wa kiroho na kijeshi aliyeuawa na Waingereza mwaka 1905.
Matakwa hayo mapya yanakuja siku chache kabla ya ziara ya mfalme Charles III nchini Kenya Oktoba 30,2023.
Samoei aliyeongoza upinzani mkali dhidi ya wakoloni ,aliuawa na mwanajeshi wa Uingereza kanali Richard Meirnertzehagen ,baada ya kuwalaghai Samoei na Viongozi wengine wa Nandi wa kuhudhuria mkutano wa mapatano.
Kulingana na gazeti la Daily Nation la nchini Kenya, wazee hao pia wanataka kurejeshwa kwa vitu vyao vya kitamaduni vilivyoibwa na kufidiwa kwa ukatili waliofanyiwa jamii wakati wa utawala wa wakoloni .ikiwa ni pamoja na mauaji ,kuwekwa kizuizini na kuwahamisha watu wa jamii ya Nandi kwa nguvu.
Fuvu la Koitalel Arap Samoei inasadikika kuwa katika mkusanyiko wa makumbusho mahali fulani nchini Uingereza.
Wazee wa Nandi mara kwa mara wamekuwa wakiomba kurejeshwa kwa mabaki hayo ya Samuel.
“Tunamsihi Mfalme Charles, tunahitaji kupata fuvu hilo lirudishwe Nandi tufanye mazishi ya heshima.
David Samoei aliliambia shirika la utangazaji la KTN mapema mwaka huu.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.