HABARI KUU.
Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi hapo awali ilithibitisha kuwa ujumbe wa HAMAS umewasili Moscow leo kwa mazungumzo, na kutangaza walikuwa wakizungumzia na “wahusika wakuu” …..kutatua mgogoro huo haraka iwezekanavyo”…
HAMAS haichukuliwi kama kundi la kigaidi na Urusi, tofauti na nchi nyingine kadhaa ikiwa ni pamoja na Uingereza na wanachama wenzake huenda mara kwa mara Moscow, lakini hii ni safari yao ya kwanza tangu mashambulizi yao ya Octoba 7,2023.
Chombo cha habari cha Urusi RIA Novosti kilisema ujumbe huo uliongozwa na kiongozi mkuu wa HAMAS Moussa Abu Marzouk ,ambaye anadhaniwa kuishi Doha,Qatar.
Picha iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii ilimuonesha akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Mikhail Bogdanov .
Lakini Israel ilisema mikono ya viongozi wakuu wa HAMAS “Imefunkwa na damu za waisrael 1,400” na kuitaka Urusi kuwatimua wajumbe hao.
Hiyo Haiwezekani kuwa na athari yoyote huko Moscow.
Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi pia imefichua kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia yuko ndani ya mji mkuu huo.
Irani ni adui mkubwa wa Israel na mtetezi wa muda mrefu wa HAMAS, lakini pia imeendeleza uhusiano wa karibu pia na Urusi.
Urusi inashiriki katika vita hivyo ,huku Warusi na Waisrael 19 wakiuawa tangu mashambulizi ya HAMAS na wengine kushikiliwa mateka au kutoweka huko Gaza.
Ikulu ya Kremlin imetangaza pia kuwa ziara ya Rais wa Palestine, Mahmoud Abbas ipo karibu.