HABARI KUU
Utafiti mpya wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) uliochapishwa Oktoba 17,2023 katika jarida la kisayansi la kimataifa la Sage ,umeonesha wagonjwa wa moyo waliowekewa Betri ya moyo (pacemaker) wamepata hatari ya kukumbwa na matatizo ya akili.
Utafiti huo ulihusisha wagonjwa 6 waliofanyiwa vipimo vya mtambo mkubwa huitwao Cathlab na baada ya kugundua hilo waliwafuata Mabingwa wa mfumo wa akili ili kutibu tatizo hilo.
Mkuu wa idara ya utafiti ya JKCI , Dkt. Pedro Pallangyo anasema
“Tumegundua wagonjwa wote walipata changamoto ya afya ya akili kwa maana kuwa hawakuwa wamejiandaa kuwekewa vifaa vya kusaidia moyo na badala yake wakawa na dalili za magonjwa ya mfumo wa akili “
Akitolea mfano, Dkt. Pallangyo anasema hivi karibuni mgonjwa aliyewekewa betri ya moyo alijirusha kutoka ghorofani na kujiua.