HABARI KUU
Rais wa Kenya 🇰🇪 Dkt. William Ruto amesema Serikali yake imepunguza bajeti ya usafiri wa nje wa Ksh bilioni 11 (Tsh bilioni 186) baada ya ukosoaji wa umma juu ya ziara zake nyingi nje ya nchi . Dkt . Ruto amesema watumishi wa umma hawataruhusiwa kuhudhuria warsha nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha uongezaji thamani ya Vito vya Voi na uuzaji katika kaunti ya Taita Taveta ,Dkt. Ruto ameagiza kwamba bajeti za usafiri kwa mihimili yote mitatu ya uongozi zipunguzwe kwa 50%.
“Tumepunguza bajeti ya usafiri kwa Ksh 11 bilioni katika wizara au idara zote na sio ksh 50 milioni kama ilivyosemwa na baadhi ya vyombo vya habari . Hakutakuwa na makongamano ya nje ,warsha “bench marking ” kwa watumishi wa umma “
Alisema Rais William Ruto.
“Nimepunguza ile hela ya kurandaranda na kuzunguka …. niliona watu wa gazeti jana wakisema nimepunguza milioni mia tano….. hapana, nimepunguza bilioni kumi na moja”
Alisema Rais William Ruto.
“Pesa ya Wakenya haiwezi kwenda kununua marinda….ati wanaenda bench marking, ati wanaenda kununua viatu…..sasa tumesema safari yoyote itakuwa ile ya kuletea Wakenya faida..
Alisema Rais William Ruto.