MICHEZO
Ripoti kutokea Colombia zinaeleza kuwa wazazi wa Mshambuliaji wa Liverpool Luis Diaz walitekwa nchini humo lakini hadi sasa mama amepatikana.
Wakati wakielekea nyumbani kwao wawili hao walizingirwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki. Tukio hilo limetokea kwenye kituo cha mafuta.
Kupitia mtandao wa X, Rais wa Colombia Gustavo Petro amethibitisha kuwa polisi wamefanikiwa kumuokoa Bi. Cilenis Marulanda lakini baba hajulikani alipo.
Naye Mkurugenzi wa polisi nchini Colombia Jenerali William Salamanca ameapa kutumia njia zozote kuhakikisha baba wa Diaz anapatikana.
Nayo klabu ya Liverpool imesema inaamini mamlaka zitasaidia kupatikana kwa mateka huyo ,huku pia Liverpool ikiwa na imani pia Diaz atatulia.
Shirikisho la mpira nchini Colombia 🇨🇴 limeeleza kusikitishwa na kitendo hicho na kuomba mamlaka zinasaidi kupatikana kwa baba huyo.