0:00
MICHEZO
Cristiano Ronaldo achekeshwa na maneno ya Mwandishi wa habari aliyekuwa akizungumzia tuzo za Ballon d’Or ya nane ya Mshambuliaji Lionel Messi na kuutafsiri kama “upendeleo “.
Ronaldo aliweka comment yake hiyo kwenye mtandao wa As Television uliomuonyesha mwanahabari Tomas Roncero ,akisema kuwa
“Habari, tulichodhani kuwa wanaenda kumpa Ballon dOr nyingine Messi, kimetokea.
Alishinda kombe la Dunia, ndio,lakini kwa penati 6. Kombe la Dunia lilikuwa miezi 10 iliopita .na sasa tuko Novemba. Messi ana Ballon d’Or nane ,lakini anapaswa kuwa nazo tano . Ana Ballon dOr ya Iniesta na Xavi,Robert Lewandowski ambaye alishinda mataji sita katika msimu mmoja na Haaland ambaye amekuwa mfungaji bora kwa kila ligi anayoshiriki”
Ronaldo ali-like chapisho hilo lenye utata ,na kuacha comment ya emoji nne za kucheka .
Comment hiyo ya Mshambuliaji wa Al-Nassr ina zaidi ya like 90,000.
Related Posts 📫
SYDNEY, - Croatia and Argentina have taken the last two...
Sababu kubwa ni kwamba tarehe hizo Baba wa Taifa hilo...
Todd Boehly has made a number of high-profile deals over...
Nollywood star Uche Jombo took to Instagram to share heartbreaking...
MAGAZETI
Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...