PAPA ATEUA MAPADRI HAWA KUWA MAASKOFU
HABARI KUU Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani, Papa Francisco amewateuwa mapadri wawili kuwa maaskofu kwenye majimbo mawili ya kikatoliki ya Njombe na Bukoba. EUSEBIO KYANDO Maaskofu hao wateule ni pamoja…
SERIKALI YAWATOA HOFU WANANCHI UPATIKANAJI WA MAFUTA
MAGAZETI
Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za magazeti ya asubuhi hii ya Octoba 20,2023.
(more…)
SIRI YA MICHAEL JACKSON YAFICHUKA
NYOTA WETU
Michael Jackson aliundiwa mfumo wa kucheza ambao ulipingana na nguvu ya mvutano . Ili kutimiza hilo alitengenezewa kiatu maalum na baadaye kupata haki miliki ya kiatu hicho.
Mafanikio ya Michael Jackson ni kama hadithi , ni msanii wa kwanza kushinda tuzo nane za Grammy usiku mmoja; pia ni msanii wa kwanza kuuza nakala zaidi ya milioni moja kwa wiki ya kwanza.
Athari ya uchezaji wake imekuwa ya vizazi kwa vizazi Ulimwengu mzima. Baadhi ya mashabiki wake wamekuwa wakijitahidi kuiga staili zake za uchezaji bila ya kufahamu ,Mfalme wa POP pengine alitumia ufundi wa kisayansi.
Lakini kuna jambo lilishangaza Ulimwengu kwa kucheza akiwa amenyooka na kuinamia mbele akipingana na Nguvu au kani ya mvutano ( gravitational force) alionyesha hivyo kwa mara ya kwanza katika video yake ya mziki ya 1988 “Smooth Criminal “. Katika onyesho hilo Jackson na wachezaji wake wachache wanaegemea mbele kwa kimo cha nyuzi 45,huku migongo imenyooka ,miguu na kushika sakafuni,na kurudi taratibu.
“Haiwezekani kimwili kufanya hivyo ” alisema Daktari wa upasuaji wa neva Dk. Nishant Yagnick ,shabiki wa muda mrefu wa Michael Jackson ambaye anafanya kazi katika Taasisi ya Uzamili ya Elimu ya Tiba na utafiti huko Chandigarh, India.
Unaweza kupinda mgongo kiwango cha juu cha nyuzi 25 hadi 30 kwenda mbele kabla ya kuanguka kifudifudi.
Wacheza Shoo waliofunzwa zaidi wanaweza kuinama kwa kiwango cha juu cha nyuzi 25 au 30 kwa kulalia mbele tena kwa bahati kubwa.
Pamoja na Jackson kuwa na umbo la kipekee katika kucheza,hata yeye hakuweza kufanya hivyo bila ujanja na msaada ,yeye na timu yake walivumbua kiatu maalum ambacho kingemtia nanga kwenye sakafu wakati wa kuinama.
Kiatu hicho chenye haki miliki ya Michael Jackson kina vifaa maalum kwaajili ya kuondoa nguvu ya uvutano na kurahisisha uchezaji ule na pia kuzuia kuanguka.
Viatu hivyo vilipewa haki miliki Octoba 26,1993 ,vina sehemu ya kisigino iliyoundwa maalumu ambayo inaweza kuunganishwa kwa urahisi na kitu kama vile jukwaa au sakafu.
Kabla ya kucheza kwa kutumia viatu hivyo unatakiwa kuwa na mazoezi ya kutosha pia na daktari wa mziki.
(more…)
WAKONGOMANI WALITAKA JESHI LA AFRIKA MASHARIKI KUONDOKA
HABARI KUU
Muungano wa vyama vya kiraia katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 umefanya maandamano mjini Goma ukitaka kikosi cha pamoja cha Afrika Mashariki kuondoka Mashariki mwa nchi hiyo kutokana na kushindwa kukabiliana na waasi wa M23.
Mwezi Novemba mwaka jana, Kenya 🇰🇪, Burundi 🇧🇮, Uganda 🇺🇬, na South Sudan 🇸🇸 zilituma wanajeshi wake DRC ,chini ya bendera ya jeshi la kikanda la Jumuiya Ya Afrika Mashariki (EACRF) ,kujaribu kulipokonya silaha kundi hilo la waasi na kuleta amani.
(more…)
WAFANYA VURUGU UBUNGO
HABARI KUU Wafanyabiashara wa soko la simu 2000 lililopo halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ,Dar es salaam mapema leo,Alhamisi Oktoba 19,2023 wameandamana sambamba na kufunga barabara wakishinikiza mamlaka za serikali…
MISRI NA MAREKANI ZAKUBALI KUFUNGUA MIPAKA
HABARI KUU.
Rais Joe Biden wa Marekani na Abdel Fattah al-Sisi wa Misri wamekubali kufungua kivuko cha Rafah ili kuruhusu hadi lori 20 za misaada kuingia Gaza.
(more…)
BARCELONA NA REAL MADRID KWENYE VITA
MICHEZO
Klabu ya Barcelona ipo kwenye vita kali na Real Madrid kuwania saini ya mchezaji wa Manchester City, Julian Alvarez.
Barca wanalazimika kurejea sokoni baada ya Mshambuliaji wao ,Robert Lewandowski kupata majeraha na kupelekea kutetereka kwa safu yao ya ushambuliaji ,jambo ambalo limefanya kuamua kuelekeza nguvu zao zote kwa Mshambuliaji huyo wa Manchester City, Julian Alvarez.
Mabingwa hao watetezi wa ligi ya La Liga walifanikiwa kuinasa saini ya kinda wa Athletico PR, Vitor Roque kutoka Brazil kabla ya Mshambuliaji huyo kupata jeraha la kifundo cha mguu ,ambapo anatarajiwa kuwa fiti kabla ya kuhamia rasmi Barcelona, mwezi Januari.
Ingawa Vitor Roque anaweza kuwa mchezaji bora katika siku zijazo,klabu hiyo itahitaji mchezaji imara ambaye anaweza kusaidiana na Lewandowski anayeelekea ukingoni.
Mshindi huyo wa kombe la Dunia na Argentina, yuko katika kiwango cha hali ya juu msimu huu baada ya kupachika mabao 6 na kutoa msaada wa goli 5 katika mechi 13 za Manchester City kwenye mashindano yote,Manchester City inashiriki Ligi kuu ya England.
(more…)
WACHEZAJI SIMBA KUPATA KIASI HIKI CHA PESA
MICHEZO Wachezaji wa Simba washindwe wao tu sasa hivi hiyo ni baada ya kuhakikishiwa kupewa pesa ya maana katika michezo miwili ya robo fainali ya AFL dhidi ya Al Ahly.…
- Go to the previous page
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- …
- 10
- Go to the next page