NYOTA WETU.
Mmiliki wa mtandao wa X,SpaceX, na Tesla Elon Musk ameonekana kuonyesha wasiw.asi wake juu ya matumizi ya Akili Bandia (Artifical Intelligence (AI)) .
Mapema mwaka huu Musk alionya kuwa teknolojia hiyo inaweza kuleta uharibifu wa ustaarabu.
Bilionea huyo yuko nchini Uingereza kwenye mkutano mkubwa wa AI uliokutanisha mabosi wa teknolojia na Viongozi kutoka pande mbalimbali za Dunia.
Akizungumza na shirika la habari la Sky News ,Musk aliulizwa kama bado anafikiria teknolojia hiyo ni tishio kwa binadamu, naye alijibu kuwa “ni hatari”.
“Bado sijaelewa vizuri kama tunaweza kudhibiti hiki kitu, lakini nadhani tunaweza kulenga kuilekeza kwenye mwelekeo zmbao utakuwa na manufaa kwa Binadamu “.
Jambo hili linajili wakati ambao nchi nyingi ikiwemo China na Marekani zikiunga mkono mpango wa Uingereza wa kushirikiana kutumia vizuri uwezo wa teknolojia hiyo ,kukabiliana na hatari zake pamoja na kulinda usalama wa raia wake.