HABARI KUU.
Kutokana na kile ambacho tunaweza kuangalia ni kwamba, Waisrael, ambao walikuwa wameanza uvamizi wa Gaza Polepole ,hivi sasa wameanza kupinga hatua kubwa.
Wanajeshi wao 17 wameuawa katika vita,na hiyo ilitokana na makombora kadhaa ya vifaru ambayo yalishambulia maeneo yao.
Jeshi la Israel (IDF) limetoa video kadhaa asubuhi ya leo za Wanajeshi katika maeneo yasiyojulikana.
Wanaonekana kuwa karibu zaidi na mji wa Gaza,lakini ni muhimu pia kukumbuka hili ni eneo dogo.
Wakati wa amani,unaweza kwenda Gaza na kuingia katikati mwa jiji la Gaza kwa takribani 15 pekee. Lakini, imewachukua wanajeshi wa jeshi la Israel siku chache kufika kwenye jiji hilo,jambo ambalo linaonyesha kuwa wanasonga Polepole.
Ni muhimu kusema kwamba huwezi kulinganisha na vita ya Urusi dhidi ya Ukraine. Haya si majeshi makubwa mawili makubwa yaliyosimama na silaha nzito nzito,yakikabiliana moja kwa moja.
Kwahiyo Hamas haitajaribu kuwa na vita vya moja kwa moja dhidi ya Waisrael. Watakachojaribu kufanya ni kuwasumbua.