NYOTA WETU
Mchekeshaji nguli wa Nigeria, John Okafor “MR IBU” amekatwa mguu jana baada ya kufanyiwa upasuaji mara saba na sasa na sasa amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi “ICU”.
Taarifa iliochapishwa na binti yake kwenye ukurasa wake wa Instagram imewaomba Wanigeria wote wamuombee dua mbali na michango ya pesa za matibabu.
“Kufikia saa saba za mchana jana, Baba yangu amefanyiwa upasuaji mara saba,hata hivyo hili kuokoa maisha yake na kuongeza uwezekano wote wa kupona,ilibidi mguu wake mmoja ukatwe.
“Tukio hili limekuwa gumu kwetu sote lakini imetubidi tukubali ukweli huu mpya wa hali ya baba ili kumuweka hai”.
Mr IBU alianza kuugua tangu Oktoba mwaka huu na alionekana kwenye video moja akiwa amelazwa hospitalini,akiomba msaada wa kifedha.