NYOTA WETU.
Taarifa kutokea Marekani zinaeleza kuwa masaa manne ya ushahidi kutoka kwa mtoto mkubwa wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump unaweza kufupishwa kwa neno moja “sikumbuki”.
Jumatano,Ivanka Trump (42) alikuwa mwanafamilia wa nne wa kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili baba yake na kaka yake.
Katika kesi hiyo, Mwanasheria wa New York anamtuhumu Trump kwa ulaghai uliompelekea kupata mikopo ya benki.
Ivanka alishikilia msimamo wake kuwa “sikumbuki” au “sijui” na kujibu kwa upole huku akitabasamu kwa kiasi hata wanasheria na majaji walipokuwa wakali.
Profesa kutokea chuo kikuu kimoja nchini Marekani ambaye ni mtaalamu wa kesi hizo amesema maneno aliyotumia binti huyo ni maneno ya mkakati wa kawaida kwenye kesi za biashara.