HABARI KUU.
Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa,ofisi ya mafundisho ya Vatican ilisema Jumatano ,ikijibu maswali kutoka kwa Askofu.
Idara hiyo, inayojulikana kama Dicastery of the doctrine of the faith ,haikuwa wazi hata hivyo,katika kujibu kuhusu wenzi wa jinsia moja wanaweza kupata ubatizo wa kanisa kwaajili ya mtoto aliyeasiliwa au yule aliyepatikana kwa mama mlezi.
Askofu Jose Negri wa Santo Amaro Brazil 🇧🇷 alituma kwa ofisi ya mafundisho maswali sita mnamo julai kuhusu watu wa mapenzi ya jinsia moja na waliobadili jinsia ( LGBTQ) na ushiriki wao katika Sakramenti za ubatizo na ndoa.
Kurasa hizo tatu za maswali na majibu zilitiwa saini na mkuu wa idara hiyo, Kadinali wa Argentina Victor Manuel Fernández, na kuidhinishwa na Papa Francis mnamo Oktoba 31.
Ziliwekwa kwenye tovuti ya idara hiyo mnamo jumatano kwa kutumia neno la kiitaliano “transsexuals “.
Papa Francis, mwenye umri wa miaka 86 ,amejaribu kulifanya kanisa liwe na ukarimu na watu wa jamii ya LGBTQ bila kubadili mafundisho ya Kanisa, ikiwa ni pamoja na msemo mmoja kwamba kuvutia watu wa jinsia moja si dhambi bali kitendo chenyewe cha kushiriki mapenzi ya jinsia moja ndio dhambi.