MICHEZO
Msemaji wa Yanga sc, Ally Shaban Kamwe amewaomba mashabiki wa klabu hiyo, siku ya jumapili asubuhi kila mmoja abebe chapati zake,maandazi,vitumbua aje navyo pale jangwani kwani supu itagawiwa bure.
“Jumapili kila mwana Yanga aje na vitumbua vyake,maandazi pamoja chapati yake ,supu tunatoa free na siku hiyo asubuhi wakati supu inapikwa kutakuwa na matembezi kidogo ya hisani,tutaanza kutembea pale Jangwani na tutatembea mpaka Msimbazi mataa then tutarudi na tukiwa njiani tutakuwa tunawasalimia kila tutakaye kutana nae njiani. Tukirudi Jangwani tutakula supu maana tumechinja ng’ombe 10 na ng’ombe mmoja anasimama kwaajili ya watu 600 na tukiamua tupeleke Mkwakwani kote wangekunywa supu na Jumapili nyie njooni na vitafunwa ,mabakuri yapo.
Amesema Meneja wa habari Ally Shaban Kamwe.