NYOTA WETU.
Luis Manuel Diaz, Baba mzazi wa Mshambuliaji wa Liverpool Luis Diaz amezungumza kwa mara ya kwanza tangu aachiliwe huru.
Akiongea kwa hisia kali na hata kulia mzee Diaz (58) alisema
“Walinilazimisha nitembee sana ,bila kupumzika vizuri,tukiwa milimani kwenye mazingira magumu sana.
Nisingetaka mtu yeyote awe kwenye mazingira ya kule milimani niliopitia mimi.
Ulikuwa wakati mgumu sana kwangu,sijalala vizuri kwa muda wa siku 12.
Watekaji walinihimiza kutulia ,japo walinihudumia vizuri lakini sikuwa na raha.
Alisema mzee Diaz huku akilia kwa uchungu.
Mzee Diaz na mke wake Bi. Cilenis Marulanda walitekwa mnamo Oktoba 28 katika mji wa Barrancas Colombia 🇨🇴.
Polisi walifanikiwa kumuokoa mama huyo masaa machache baadae, huku watekaji wakiendelea kumshikilia mzee Diaz.