NYOTA WETU.
Haya ndio maisha ya mwanasoka feki ambaye alijifanya kuwa ni mchezaji wa Ligi ya EPL hadi kufanikiwa kuwadanganya watu wengi hasa wanawake akiwemo mke wa nyota wa zamani wa soka Thierry Henry.
Kupitia ulaghai huo alikuwa akijipatia maelfu ya pauni,aliishi maisha ya anasa ,akitumia magari na majumba ya kifahari.
Medi Abalimba alizaliwa nchini DRC ,akiwa na umri wa miaka mitano yeye na familia yake waliamia nchini Uingereza kwenye mgogoro wa kivita nchini mwake mwaka 1990.
Abalimba alijaribu kuishi kifahari kama wanasoka wa kimataifa. Mhalifu huyu analaumu
Uanasoka ulikwama ikiwa ndio sababu ya kuwa mdanganyifu
Aliwahi kujifanya nyota wa zamani wa Chelsea Gael Kakuta,vilevile aliwahi kukodi helicopter akawachukua wasichana wanne kutokea Manchester akawazungusha jijini London na baadaye kuwafikisha kwenye nyumba ya kifahari aliyodanganya kuwa ni ya kwake.
Manunuzi yake ya vitu vya kifahari dukani ndiyo yalimfanya akamatwe kwani mpelelezi mmoja ndani ya duka fulani alimshtukia na kuwaita polisi.
Uchunguzi ulifanyika na alifungwa kwa muda wa miaka minne baada ya kukiri mashtaka ikiwemo kuchukua gari aina ya Range Rover bila idhini.
Akiwa jela,aliingia kwenye mahusiano na muuguzi mmoja ambaye alimletea simu kwa siri gerezani. Uhusiano wao uligundulika na mwana mama huyo alihukumiwa kifungo cha miezi 20 kwa utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma.
Kwa simu hiyo aliyopewa na muuguzi akiwa jela Abalimba alikuwa akiongea na mke wa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Thierry Henry (Bi.Claire Merry) kila siku kwa miezi kwa miezi minne huku akijifanya yuko jeshini Kuwait 🇰🇼.
Abalimba aliachiwa mwaka 2018 na aliendelea na uhalifu. Aliingia kwenye uhusiano uliodumu kwa wiki sita na Mwanamke mmoja maarufu na kumuibia pauni 32,000.
Baadae alipanga na kukutana na Bi Claire Merry ambaye alifanikiwa kumlaghai kiasi cha pauni 50,000.
Alikamatwa tena na baadaye kukiri makosa yote 15 yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo kosa la kutumia leseni ya udereva wa kughushi na kadi feki ya benki. Mwaka 2021 alihukumiwa kifungo kipya cha miaka minne.
Katika miaka 10 iliopita ,Abalimba alishadai kuwa mpelelezi, nyota wa England, wakala wa soka ,Mchezaji wa kikapu nchini Marekani, mwanamziki na Mwanajeshi.
Abalimba ana madeni makubwa, hata hivyo hana mali yoyote chini ya jina lake hali ambayo imeleta ugumu kwani hakuna fidia iliyoweza kulipwa kwa waathirika wa ulaghai wake.
Yote haya na mengine yataonekana kwenye filamu mpya itakayoruka kwenye filamu mpya itakayoruka kwenye kituo cha runinga cha ITV cha Uingereza, ambacho tayari kimeipa jina filamu hiyo kwa jina la “Cons and Swindles”.