MICHEZO.
Kocha wa Real Madrid, Mkongwe, Don Carlo Ancelotti amezungumzia makosa ambayo makocha wa kizazi kipya wanafanya kwa wachezaji wao ambapo ameelezea utoaji wa maelekezo wakati mchezaji akiwa na mpira na pale ambapo hana mpira.
Kocha huyo ambaye ni mshindi mara nne wa ligi ya Mabingwa Ulaya amebainisha kuwa kumpa mchezaji maelekezo mengi pindi awapo na mpira uwanjani ni kumuondolea ubunifu.
“Kosa wanalofanya makocha wa kizazi kipya ni kutoa maelekezo mengi kwa mchezaji pindi anapokuwa na umiliki kwa mpira awapo mchezoni.
Hii inaondoa ubunifu . Kumpa mchezaji maelekezo kuhusu nafasi awapo uwanjani akiwa hana mpira ni jambo zuri maana hapo lazima utoe maelekezo ya kutosha kwasababu akiwa hana mpira kinachozingatiwa ni umakini ,kujitolea na kucheza kwa umoja.
Mchezaji akiwa na mpira inategemea na ubunifu wa mchezaji huyo. Ikiwa Vinicius au Rodrygo wanahisi ni vizuri zaidi kufungua zaidi uwanja wakati wana mpira,sitawaambia wabaki ndani;kwasababu tafsiri binafsi ya mchezaji kuhusu mchezo “.
Amesema kocha huyo mkongwe ,Don Carlo Ancelotti.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.