MICHEZO.
Related Content
Klabu ya Al-Nassr Fc ya Saudia Arabia imefungua mazungumzo na nyota wa Ureno ,Cristiano Ronaldo juu ya nyongeza ya mkataba mpya wa kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka 2027.

Mkataba mpya huo unatarajiwa kuanza Januari 2025 na kutamatika Januari 2027.
Hivyo Ronaldo anaweza kupata nafasi ya kushiriki kombe la Dunia 2026 akiwa mchezaji wa Al-Nassr Fc.
Ikumbukwe, mkataba huo mpya wa Cristiano Ronaldo utamalizika mwezi mmoja kabla ya mshindi huyo mara 5 wa Ballon d’Or kutimiza miaka 42.