0:00
HABARI KUU.
Jeshi la Israel limefanya operesheni dhidi ya Hamas iliyolenga hospitali moja kwa moja ya Al shifa mjini Gaza . Jeshi hilo limetaka kujisalimisha kwa watu linalowaita magaida.
Mtu aliyekuwa kwenye hospitali ya Al-shifa amemwambia mwandishi wa BBC kwamba wanajeshi wameanza kuivamia.
“Askari walianza kwa kurusha bomu la machozi ambalo lilisababisha watu kukosa hewa”
Niliona wanajeshi wakiingia kwenye idara maalumu ya upasuaji “.
Amesema Khared Al-zaanoun
Hii ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Israel wameingia ndani ya hospitali ya Al-shifa baada ya siku kadhaa za mashambulizi na mapigano makali huko Gaza.
Al-shifa ndiyo hospitali kubwa huko Gaza , na Israel na Marekani zinadai Hamas ina kambi yake huko ,huku Hamas ikikanusha vikali.
Related Posts 📫
Tiger Woods will not compete in the Dec. 5-8 Hero...
HABARI KUU
Kiongozi wa Azimio, Raila Odinga ameeleza majukumu ambayo...
MAGAZETI
Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
HABARI KUU
Watanzania wawili na raia mmoja wa Afrika kusini...