HABARI KUU.
Mwanaharakati wa Chama cha upinzani cha Citizens Coalition for change (CCC) kutoka Zimbabwe aliyeteka nyara jumamosi iliyopita,amekutwa akiwa amefariki.
Msemaji wa Chama cha CCC Promise Mkwananzi ameelezea kuwa Tapfumaneyi Masaya alitekwa na watu wasiojulikana wakati akifanya kampeini,alifungwa na kuingizwa kwenye gari,baadaye aliteswa na mwili wake ulitupwa nje ya jiji la Harare.
Kulengwa kwa Bw. Masaya ni sehemu ya mfululizo wa utekwaji nyara wa wanaharakati mbalimbali nchini humo kuelekea uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Desemba 9.
Takribani wiki mbili zilizopita Mbunge wa Chama cha CCC Takudzwa Ngadziore alinusurika baada ya kutekwa na watu wenye silaha ,kuteswa na kutupwa takribani kilomita 30 kutokea Harare.
Mwananzi amewahimiza polisi kufanya kazi yao na kuhakikisha watekaji wote wanafikishwa Mahakamani mara moja na kuchukuliwa hatua ipasavyo.
Zimbabwe 🇿🇼 ina historia ya wanaharakati kupitia mitanziko ya mara kwa mara na wengine kufikia hatua ya kuuliwa.
Wapinzani wamekuwa wakilaumu chama tawala cha Zanu-PF kwa kuhusika na utesaji na vifo vya wanaharakati.