HABARI KUU.
Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Lohannis, amewasili nchini kwa ziara ya kitaifa kuanzia leo tarehe 16 oktoba hadi Oktoba 19 Novemba 2023 kufuatia mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alipowasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angela Kairuki (Mb).
Lengo la ziara hiyo ni pamoja na kushawishi uwekezaji zaidi na kuvutia utalii au watalii wengi kutoka nchini Romania 🇷🇴.
Aidha katika mazungumzo rasmi yatakayofanyika tarehe 17 Novemba 2023 Rais huyo na mwenyeji wake watajadili namna bora ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya elimu,afya,kilimo,nishati na madini.
Kabla ya kuondoka nchini mnamo Novemba 19,2023 Rais wa Romania atapata fursa ya kwenda Zanzibar ambapo atazungumza na Rais Dkt. Hussein Alli Mwinyi na kutembelea mji mkongwe ambao ni moja kati ya vivutio vikubwa vya kitalii Duniani.