HABARI KUU
Waraka mpya uliotiwa saini na Papa Francis, umesema mafundisho ya Ukatoliki na uanachama wa Freemason hayawezi kuendana .
Barua hiyo iliotolewa na ofisi ya mafundisho ya Vatican ilinukuu tamko lililotolewa miaka 40 iliopita ,likisema kwamba Wakatoliki waliojiunga na chama cha Freemason hawaruhusiwi kushiriki katika ekaristi takatifu.
Uamuzi huo wa huvi karibuni unaonekana kumjibu Askofu kutoka Ufilipino ambaye alionyesha wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa idadi kubwa ya washiriki kwenye jimbo lake kujiunga na Freemason.
Barua hiyo kuhusu Freemason ilinukuu barua au tamko la mwaka 1983 ,lililoitwa saini na Papa Benedicto XVI ,wakati huo mkuu wa mafundisho ya Vatican, likisema kwamba Wakatoliki:-
“Katika vyama vya Kimasoniki wako katika hali ya dhambi kubwa na huenda wasipate ushirika Mtakatifu “.