NYOTA WETU.
Msanii aliyejulikana zaidi kwenye miondoko ya singeli maarufu kama D Voice ametambulishwa rasmi kama msanii mpya wa lebo ya WCB.
Mmiliki wa lebo hiyo Mwanamziki Naseeb Abdul “Diamond Platinumz ” amesema walikuwa na miezi takribani tisa kumuandaa msanii huyo hili wapate zao lao pia haikuwachukua ugumu kwakuq ana kipaji na lebo ilikuwa na shauku ya kuwa na Msanii mpya.
Msanii huyo ametambulishwa katika hafla maalumu iliyoitwa Swahili Night 🌙 ambapo watu maarufu mbalimbali waliojitokeza huku watangazaji Lilly Ommy na Ammy Girl wakiongoza hafla hiyo usisahau Dvoice katika utambulisho wake imeachiwa album yake yenye nyimbo 10 zenye vionjo tofauti tofauti ukiachana na singeli, Album inaitwa “Swahili Kid” ambayo inapatikana kwenye mitandao yote ya kijamii.