MICHEZO
Siku moja tangu kamati ya kusimamia na kuendesha bodi ya ligi kuu (TPLB) kutangaza kumfungia kiungo wa Yanga, Khalid Aucho kwa kumfungia michezo mitatu na faini ya 500,000 (laki tano) kwa kosa la utovu wa nidhamu, mabosi wa klabu hiyo wapo kwenye mchakato wa kukata rufaa.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano wa klabu ya Yanga, Rogers Gumbo amesema uongozi haujakubaliana na uamuzi wa kamati hiyo ya bodi kwa kiungo huyo ambaye amehukumiwa mara mbili kinyume na kanuni zilizopo kwasasa.
Gumbo amesema wanalazimika kukata rufaa kutokana na kuwa waliwahi kuiandikia bodi ya ligi siku za nyuma juu ya beki wa Simba, Henock Inonga aliyefanya kosa kama hilo, lakini walijibiwa mwamuzi alishachukua uamuzi ndani ya mchezo kwa kumuonyesha kadi ya njano ,lakini safari hii kwa Khalid Aucho limesahaulika ,amesema kiongozi huyo.