HABARI KUU
Wizara ya sheria ya Urusi imewasilisha ombi kwa Mahakama kuu ya nchi hiyo kupiga marufuku shughuli za kile kinachoitwa “vuguvugu la kimataifa la LGBTQ ” Kama lenye itikadi kali.
Haiko wazi kama taarifa ya Wizara inarejelea jumuiya LGBTQ kwa ujumla au Mashirika ya umma.
Ilisema vuguvugu hilo limeonyesha dalili za “shughuli zenye itikadi kali” ikiwa ni pamoja na kuchochea “migogoro ya kijamii na kidini”.
Marufuku hiyo inaweza kumuacha mwanaharakati yeyote wa LGBTQ katika hatari ya kufunguliwa mashtaka ya jinai.
Hatua hiyo yenye msimamo mkali imekuwa ikitumiwa hapo awali na mamlaka za Urusi dhidi ya Mashirika ya kutetea haki za binadamu na makundi ya upinzani kama vile wakfu wa kupambana na ufisadi wa Alexel Navalny.
Mahakama ya juu zaidi itachunguza hilo mapema mwezi Novemba 30.
Marufuku hiyo ingefanya Mashirika ya LGBTQ kutokuweza kufanya kazi na kuwaweka Wanaharakati na wafanyakazi katika hatari ya kufunguliwa mashtaka ya jinai ,gazeti la Moscow Times limenukuliwa kwa kauli ya mtu mmoja wa wanaharakati wachache wa LGBTQ ambaye bado wako ndani ya Urusi akisema
“Kimsingi, itahusisha mashtaka ya jinai kwa kuzingatia tu mwelekeo au utambulisho wa mtu “.