AFARIKI AKIFANYA UPASUAJI WA KUONGEZA MAKALIO

0:00

HABARI KUU

Maofisa wa Uingereza na Uturuki watakutana kujadiliana kuhusu mfumo wa udhibiti kufuatia kifo cha Mwanamke mmoja mwaka 2019 kilichotokea katika upasuaji wa kuongeza makalio.

Melissa Kerr alifariki Dunia jijini Istanbul mara baada ya kufanyiwa upasuaji uliohusisha kukusanya mafuta na kuyaweka kwenye makalio yake.

Kifo cha Melissa (31) kilitokana na mafuta aliyochomwa kwenye makalio aliyochomwa kuingia kwenye mishipa na baadaye kwenda kuziba ateri ya mapafu.

Sababu ya kifo chake ilirekodiwa kuwa kuwa ni kuziba kwa ghafla kwa mishipa ya damu kulikotokana na kuwekewa mafuta. Huku sababu kuu ikiwa ni upasuaji wa urembo.

Maafisa hao wanaeleza kuwa Melissa hakuwa amepewa taarifa za kutosha kuhusiana na hatari za upasuaji huo ikiwemo kiwango cha vifo.

Vilevile wamesema yawezekana hakuna kabisa udhibiti au upo kidogo sana kuhusiana na upasuaji wa urembo.

Wizara ya Mambo ya nje ya Nchi ya Uingereza imeeleza inazo taarifa hizo zaidi ya raia wake 25 walipoteza maisha nchini Uturuki tangu January 2019 baada ya kufanyiwa upasuaji wa aina mbalimbali.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  MERCY CHINWO AND HUSBAND REVEAL THEIR SON'S FACE
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading