MICHEZO
Huenda Manchester United wakashindwa kushiriki kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao ,ikiwa watamaliza chini ya klabu ya OGC Nice ya Ufaransa, baada ya Sir Jim Ratcliffe kunyakua 25% za umiliki wa klabu hiyo.
Ugumu huo unasababishwa na umiliki wa Sir Jim Ratcliffe na Ineos Group ambao pia wanamiliki klabu ya Nice ya Ufaransa, ambayo kwasasa inashika nafasi ya pili kwenye Ligi 1, wakiwa pointi moja nyuma ya PSG
Kufuatia mfumo mpya wa Ligi hiyo,utakaoanza kwenye msimu ujao,pamoja na sheria za UEFA kuhusu timu tofauti zinazomilikiwa na mmiliki mmoja ,njia pekee kwa Manchester United kushiriki kwenye michuano hiyo,ni kama watamaliza nafasi ya juu zaidi kwenye premier league, kuzidi OGC Nice ya Ufaransa.
Kwa maana rahisi ni kwamba, ili United afuzu ,anatakiwa kumaliza nafasi ya tatu za juu halafu Nice amalize kwenye nafasi ya nne kwenda chini. Kama Nice atamaliza juu ya Manchester United basi,United hawatashiriki kwenye michuano hiyo,msimu ujao.
Na kama wawili hao watamaliza nafasi moja (mfano wote wamalize nafasi ya 3) kwenye ligi zao ,basi Manchester United itafuzu kutokana na Ligi kuu ya England kuwepo kwenye viwango vya juu vya UEFA kuliko ligi ya Ufaransa (Ligi 1).
Njia pekee ya wawili hao kufuzu kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya, ni kama mmoja atafuzu UEFA Champions League na mwingine atafuzu UEFA ndogo au European Conference Le