NYOTA WETU
Mtengeneza maudhui maarufu Duniani kupitia mtandao wa YouTube kwa jina la Mr Beast ,wiki hii amekuwa gumzo mtandaoni kwa kufanya maajabu ya kuzikwa na kufufuka baada ya siku saba.
Mwanablog huyo ambaye ndiye mtengeneza maudhui tajiri zaidi Duniani kwenye jukwaa la YouTube inasemekana alizikwa akiwa hai na video za moja kwa moja kurekodiwa kwenye tukio hilo.
Mtengeneza maudhui huyo inasemekana alilenga kupata wafuasi zaidi kwenye mtandao huo ambao wamekadiriwa kufika bilioni 200 ambayo inafanya kuwa mtengeneza maudhui tajiri anaelipwa na mtandao huo wa Google kiasi kikubwa cha hela.
Mr Beast kwenye video yake kama ambavyo wafu huzikwa na nguo nyeusi alifuata mtindo huo huo huku jeneza lake likipambwa kwa kioo sehemu ya juu ya kioo kilichomuonesha akiwa ndani ya kaburi lake la siku saba.
Ndani ya jeneza hilo alilowekwa kwa siku saba kulikuwa na taa,maua ,vyakula na hata vinywaji huku marafiki zake wakicheza na kuimba kuzunguka eneo ambapo alikuwa amezikwa ili aweze kutoka.
Licha ya kuzikwa na kulala kwenye jeneza kwa siku saba .mtengeneza maudhui huyo alitoka ndani ya kaburi akiwa mzima ,hii kwake ni mara ya pili kufanya hivyo akiwa katika harakati za kuongeza wafuasi kwenye mtandao huo wa You
kutoka