NYOTA WETU.
Tochukwu Ojogwu ,Rapa maarufu wa nchini Nigeria 🇳🇬 kwa jina maarufu “Odumodu ” amefichua ni kiasi gani cha fedha ambacho mwimbaji na mshindi wa tuzo za Grammy, Temilade Openiyi “Tems” anatoza kwa kolabo.
Odumodu katika andiko lake kwenye mtandao wa X siku ya Ijumaa, Novemba 24,2023 ,aliweka wazi kuwa kufanya kolabo na Tems kunagharimu dola 500k sawa na Tsh. Bilioni 1.25 .Huku Tems akijibu kwa kusema “samahani,muache TEMS apumue” akiwa na maana huenda kiasi hicho cha pesa ni kikubwa mno alichokitaja Odumodu.
Hii inakuja baada ya kuulizwa ikiwa muimbaji huyo Tems atashirikishwa kwenye “deluxe edition” kutoka kwenye album yake ya “Eziokwu” . Iliyopangwa kutoka Ijumaa, DISEMBA 1,ikiwa imejumuishwa kolabo kadhaa kutoka kwa Black Sheriff, Nasty C,Teni,Mizzle,BOJ,Duncan Mighty, Reeplay na wengine.