NYOTA WETU.
Neymar Jr na mpenzi wake,Bruna Biancardi wametengana mwezi mmoja tu baada ya kumkaribisha mtoto wao wa kwanza aitwae Mavie.
Uamuzi huo umekuja baada ya uvumi katika wiki za hivi karibuni kwamba hawapo tena pamoja ,huku kukiwa na tetesi za Neymar kutokuwa mwaminifu kwa mzazi mwenzie.
Biancardi mwenye umri wa miaka 29 ,alithibitisha ujumbe huu kwenye Insta story akisema
“Hili ni suala la faragha, lakini kwa kuwa mara nyingi nahusishwa na habari ,tuhuma na utani, ningependa kuwajulisha siko kwenye mahusiano. Sisi ni wazazi wa Mavie ,na hii ndio sababu ya Muungano wetu”.
Ripoti zinadai wawili hao wawili walikuwa na mkataba wa ajabu ambao ulimruhusu Neymar kutaniana na kulala na wanawake wengine kwa masharti maalumu ya mkataba ikiwa ni pamoja na Mbrazil huyo hakuruhusiwa kuwabusu wanawake wengine mdomoni na atalazimika kutumia kondom wakati wa tendo la ngono,na kwamba uhusiano huo unatakiwa kuwa wa siri.