KISSINGER AAGA DUNIA

0:00

NYOTA WETU

Mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani ambaye aliwahi pia kuwa Waziri wa mashauri ya kigeni ya nchi hiyo,Dkt. Henry Alfred Kissinger amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 100 huku Ulimwengu wa siasa nchini humo ukimkumbuka.

Kissinger ambaye aliwahi kuwa Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani na mshauri wa masuala ya usalama wa nchi hiyo chini ya utawala wa Marais,Richard Nixon na Gerald Ford, amefariki akiwa kwake huko Connecticut siku ya jumatano.

Mwaka 1973 Kissinger alitunukiwa Tuzo ya amani ya Nobel,kwa kujadili kumaliza vita ya huko Vietnam.

Hata hivyo yeye na Rais Nixon walikumbwa na ukosoaji mkali wa washirika wa Marekani kufuatia anguko la Saigon mnamo April 30,1975 wakati vikosi vya Vietnam 🇻🇳 Kaskazini vilipoiteka Saigon ambayo kwasasa inajulikana kama Ho Chi Minhi City.

Mabinti wawili wa Rais Nixon, wamemtaja Kissinger ambaye alishirikiana na baba yao kwenye vita ya Vietnam kama “mwanadiplomasia wa hali ya juu nchini Marekani “.

Rais wa Zamani wa Marekani, George W Bush amemtaja Dkt. Kissinger kama

“Mmojawapo wa sauti zinazotegemewa na za kipekee kuhusu mambo ya nje ya nchi”.

Dkt. KISSINGER ameacha mjane wa karibu miaka 50 ,Nancy Maginnes Kissinger, na watoto wawili wa ndoa yake ya kwanza,David na Elizabeth na wajukuu watano.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading