NYOTA
Muigizaji wa muda mrefu nchini ,Wema Sepetu amefunguka wazi na kuelezea kuwa wanaume wengi hawapendi tabia za wapenzi wao kuwaomba pesa kwa kusudi la kupima upendo wao wa kweli.
Kulingana na ,Wema,kumekuwa na tabia nyingi kutoka kwa wanawake kutoamini upendo wa kweli wa wapenzi wao jambo ambalo wameiweka kasumba ya kuitisha wanaume wao hela ovyo ovyo ili kutambua iwapo wanapendwa.
“Wanaume wengi hukerwa na tabia za wanawake kuitisha hela kila mara kwa kusudi la kupima iwapo wanaume wao wanawapenda ,jambo hili limewafanya wanawake wengi kutoamini mapenzi ya kweli kwa kuleta kasumba ya kutambua uwepo wa mwanaume kwa kumuomba pesa.
Wanawake msije mkajipendekeza kwa wanaume kwasababu ya pesa zao ikiwa kuna upendo wa kweli kila mwanaume anajua majukumu yake ya kulinda mke wake na familia bila kushawishiwa kutoa pesa”.