HABARI KUU
Kaimu wa Rais ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kasim Majaliwa amewahakikishia watanzania kuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango ni mzima wa afya na yupo ziara ya kikazi nje ya nchi.
Majaliwa ambaye kwasasa anakaimu nafasi ya Urais baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa nje ya nchi akihudhuria mkutano wa uhifadhi wa mazingira unaofanyika Dubai kwenye falme za kiarabu na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa nje ya nchi kikazi kwa mujibu wa Majaliwa Kasim Majaliwa, amenukuliwa na gazeti la Nipashe kuwa Watanzania wasiwe na wasiwasi wowote kwa kuwa Makamu wa Rais yupo ziarani kikazi nje ya nchi. Pamoja na kauli hiyo,Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa akuitaja nchi aliyopo Makamu wa Rais.
Ikumbukwe mara ya mwisho Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango kuonekana ilikuwa mwezi Oktoba.