MICHEZO
Mchezaji wa Manchester City, Erling Haaland huenda akaadhibiwa na chama cha soka England baada ya kumkashifu mwamuzi Simon Hooper kufuatia sare ya 3-3 dhidi ya Tottenham Hotspurs ,siku ya jumapili, Desemba 3.
Haaland alicharuka baada ya Hooper kusitisha maamuzi ya faida kwa Jack Grealish kuwa sehemu sahihi huku wachezaji wenzake wakipata mshangao.
Baada ya mchezo kumalizika ,Hooper alizingirwa na wachezaji wa Manchester City, huku Haaland akiongeza mchecheto hasa kwenye mitandao yake ya kijamii kwa kutumia kauli chafu .