HABARI KUU.
Kampuni ya Spotify ambayo ni watayarishaji wa mziki kutokea Sweden imetangaza kukata asilimia 17 ya wafanyakazi wake kwa lengo la kubana matumizi.
Kampuni hiyo ina wafanyakazi wapatao 9,000 ,na punguzo ill litahusu wafanyakazi wapatao 1,500.
Mkurugenzi mkuu wa Spotify Daniel Ek amesema amelazimika kufanya maamuzi magumu kwani kwasasa ukuaji wa uchumi ni hafifu.
“Najua punguzo hili litaleta maumivu makali kwenye timu ,haswa kwa watu wengi wenye mchango mkubwa kwenye kampuni,lakini hatuna budi kufanya hivyo ili kuweza kufikia malengo.
Niwe mkweli, vijana wenye werevu,wenye talanta na wachapakazi watatuacha”.
Mwanzoni mwa mwaka huu,kampuni hiyo yenye lengo la kufikia watumiaji bilioni kufikia 2030 ilipunguza kundi lingine la wafanyakazi.