NYOTA WETU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi walioorodheshwa katika jarida la Forbes la wanawake wenye uwezo mkubwa Duniani 2023 ,akipanda nafasi mbili kutoka 95 mpaka 93.
Kwa mujibu wa jarida hilo, safari hii ameingia tena kwenye orodha hiyo akiwa Mwanamke kutokea Africa kuhutubia Baraza la umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2021 ,alikuwa mwanamke kiongozi wa tano wa kiafrika kuhutubia Baraza kuu la umoja wa Mataifa. Pia alitumia ushawishi wake kwa kuikosoa Dunia kwa jinsi chanjo ya Covid ilivyokosa usawa.
Dkt. Samia Suluhu Hassan amejitofautisha Duniani kwa aina ya uongozi wake na mtangulizi wake kwa kufuata itifaki zote za Covid ,ikiwepo kuwapa kalantini wageni wanaotoka nchi zenye janga la Covid.
Rais Samia Suluhu Hassan, amekuza mahusiano ya kimataifa na kidplomasia jambo ambalo mpaka sasa limeleta mafanikio makubwa kwa nchi ya Tanzania kutembelewa na marais wa nchi nyingi katika muda mfupi wa uongozi wake.