HABARI KUU
Jumla ya wagombea wanne wa urais nchini CONGO wamejiengua kwenye mchakato wa kinyang’anyiro cha kugombea urais wa CONGO na kuamua kumuunga mkono ,Gavana wa zamani wa jimbo lenye utajiri wa madini ,Moise Katumbi “Chapwe” ambaye ni mgombea wa upinzani.
Wanasiasa waliojitoa kwenye mchakaro huo ni; Delly Sesanga,Matata Ponyo, Seth Kikuni na Franck Diongo. Hatua hiyo inafanya wagombea waliosalia kuwa ni 21 na wote wanachuana dhidi ya Rais Felix Tshisekedi anaewania muhula wa pili wa urais.
Kampeini zilianza wiki mbili zilizopita na zinatarajiwa kuitimika mnamo Desemba 18,2023 siku mbili kabla ya uchaguzi kufanyika kwenye nchi hiyo ya Afrika Mashariki yenye watu wanaokadiriwa kuwa milioni 9
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.