MICHEZO.
Kundi la mashabiki wa Arsenal wameanzisha ukurasa maalamu wenye jina la “GoFundMe ” ili kukusanya kiasi cha paundi Milioni 25 (Bilioni 79 TSH) ili kuilipa West ham pesa zaidi ya usajili wa mchezaji huyo , Declan Rice aliwashangaza wengi alipofunga bao la jioni dhidi ya Luton kwenye ushindi wa 3-2 na kuipaisha Arsenal mpaka kwenye kilele cha ligi ya Uingereza.
Mashabiki hao wa Arsenal wanaimani kuwa Wagonga Nyundo hao wa London ,walitapeliwa kwa kumuuza Declan Rice kwa ada ya usajili ya paundi milioni 105,bei inayomfanya kuwa mchezaji ghali namba 3 kusajiliwa kwenye ligi ya premier.
Rice mwenye umri wa miaka 24,alijiunga na Washika Mtutu wa London kwa kiasi cha paundi Milioni 105 sawa na bilioni 331.1 msimu uliopita wa majira ya joto,amekuwa mchezaji tegemeo kwenye kikosi cha meneja ,Mikel Arteta.