MICHEZO
Real Madrid wameripotiwa kupanga kutuma ofa ya mwisho kwa nyota wa Paris-Saint Germain , Kylian Mbappe mwezi January 2024,lakini watapata muda wa hadi tarehe 15 ya mwezi huo kufanya mustakabali wake.
Kwa mujibu wa AS,Mbappe atakuwa huru kufanya mazungumzo na Mabingwa hao wa kihistoria wa Ulaya kwani mkataba wake na PSG utakuwa unamalizika kwenye majira ya joto na atakuwa tayari kufanya mazungumzo na Madrid.
Ikiwa Mshambuliaji huyo Raia wa Ufaransa hatafikia makubaliano na Madrid, huenda Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland akawa kwenye rada za Los Blancos .
Mfaransa huyo, anayetajwa kama mchezaji bora kuwahi kutokea Duniani, amekuwa akihusishwa na Real Madrid kwa kipindi cha miaka 6 toka alivyofanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.