NYOTA WETU.
Sean Combs “Diddy ” ameshtakiwa kwa ubakaji na ulanguzi wa ngono kwa msichana wa shule mwenye umri wa miaka 17,alipokuwa darasa la 11 katika madai ya nne ya unyanyasaji wa kingono.
Hili ni shitaka la nne kwa nguli na bilionea huyo wa mziki Duniani ndani ya wiki tatu akishitakiwa kwa unyanyasaji wa kingono, ambapo hivi karibuni pia aliruka kiunzi kama hicho kwa mwanamziki wake wa zamani, Cassie, ambapo inasemekana walimalizana kwa malipo ambayo hayakujulikana ni kiasi gani cha pesa.
Katika taarifa yake Combs aliandika “INATOSHA”.
“Kwa wiki kadhaa zilizopita, nimekaa kimya na kutazama watu wakijaribu kuua “tabia” yangu,kuharibu sifa yangu na urithi wangu.
Madai ya kuhudhi yametolewa kwangu na watu wanaotaka malipo ya haraka .
Nimesema wazi: Sikufanya chochote cha kuhuzunisha kinachodaiwa. Nitapigania jina langu,familia yangu na ukweli”.
Mshtaki wa sasa anadai alikuwa na umri wa miaka 17 alipodungwa sindano ya madawa na kubakwa na Combs,msaidizi wake wa muda mrefu Harve Pierre, na Mwanaume mwingine ambaye bado hajatajwa ,mnamo mwaka 2003.
Jarada hilo limejumuisha picha ya mshtaki,anayejulikana kama “Bi Doe” akiwa ameketi kwenye mapaja ya Combs ,wakati huo akiwa na umri wa miaka 34 , na anadai shambulizi hilo lilimsababishia “mshtuko mkubwa wa kihisia na hisia za aibu ambazo zinamkumba karibu kwenye maisha yake yote kwa zaidi ya miaka 20.