MICHEZO
Bosi wa klabu ya Chelsea, Toddy Boehly , amedhamiria kuweka rekodi kwa kumsajili nyota wa Nigeria na Mshambuliaji wa Napoli ya Tulin , Victor Osimhen ,wakati wa dirisha la usajili litakalofunguliwa, mwezi Januari.
Osimhen amekuwa kwenye rada za Arsenal, lakini huenda Washika Bunduki wa London wakaachana na dili lake, baada ya Napoli kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa ,huku Rais wa klabu hiyo Aurelio De Laurentiis akitumaini Osimhen atasaini mkataba mpya, licha ya uhusiano wake na klabu yake kuzorota kwa siku za hivi karibuni.
Hata hivyo, Chelsea inafukuzia dili hilo kwa klabu mno huku ikiwa kwenye mahesabu makali ya hata kumuuza Mshambuliaji wake,Armando Broja hili kupata pesa zaidi za kumsajili Mnigeria huyo mwenye thamani ya paundi milioni 100 sokoni.
Aidha, mkataba wa Osimhen unatamatika 2025,Napoli watahitaji kumshawishi Mnigeria huyo asalie klabuni hapo kabla ya dirisha kubwa la usajili hili kuepuka kumpoteza bure ifikapo msimu wa 2025.