NYOTA WETU.
Rapa BlueFace alikaa kwenye mahojiano kwa muda usiozidi sekunde 30 na mchekeshaji maarufu, Funny Marco,mnamo siku ya Desemba 5,2023.
BlueFace alisusia mahojiano hayo baada ya kugundua mwendeshaji wa kipindi hicho hana taarifa kuhusu yeye . Funny Marco alimuuliza BlueFace ni kwanini akirap anakuwa nje ya beats?
Rapa huyo mwenye umri wa miaka 26, alimuuliza mchekeshaji huyo wa mitandaoni,
“Wimbo gani wangu ambao umesikia nimetembea nje ya beats?”.
Wakati Funny Marco akikosa majibu ya moja kwa moja ,BlueFace alimtaka Mtayarishaji wa mahojiano yao kutaja nyimbo tatu ambazo alitembea nje ya beats na akishindwa ,mahojiano yatakuwa yamefika mwisho
“Bust down Thotiana featuring Cardi B”
Funny Marco alijibu
Lakini jibu lake halikumfanya BlueFace aendelee kuwa huru na mahojiano hayo na baadaye aliondoka na kumuacha mtangazaji huyo.
Hapa Tanzania, hivi karibuni Baraka Da Prince alisusia mahojiano na kituo cha redio cha Mjini Fm wakati akienda kuzindua wimbo wake mpya “Goodbye “. Aliondoka baada ya kuulizwa swali kuhusu Ali kiba.