HABARI KUU
Nchini Burkina Faso, utawala wa mpito unaoongozwa na Ibrahim Traore umepitisha muswada wa marekebisho ya katiba na hivyo kutangaza lugha zao za ndani kuwa lugha zao rasmi baada ya sasa Kifaransa kushushwa hadhi rasmi kuwa “lugha ya kazi”.
Ripoti ya Baraza la Mawaziri inabainisha kuwa muswada huu “ni sehemu mojawapo ya utekelezaji wa majukumu makuu ya mpito ambacho ni kufanya mageuzi ya kisiasa,kiuadilifu na kiutawala kwa lengo la kudumisha utamaduni wa kidemokrasia na kuimarisha utawala wa kisheria”.
Miongoni mwa mafanikio makubwa ya nakala hii mpya ni kuhainisha lugha zao za ndani kuwa lugha rasmi badala ya Kifaransa ambayo kwasasa inaenda kuwa lugha ya kazi.
Mapema mwaka huu,Mali,inayoongozwa kama Burkina Faso na jeshi imekuwa na mahusiano mabaya na Ufaransa, ilibadilisha katiba yake kupitia maoni na kutoa hatma sawa kwa Kifaransa.
Muswada huu,ambao bado lazima upigiwe kura na Bunge la mpito ,pia unapendekeza “kuanzisha mifumo ya kutatua migogoro ya jadi na mbadala”.