HABARI KUU
Mwaka huu unatajwa kuwa mwaka wenye joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa kulingana na huduma ya Mabadiliko ya hali ya hewa ya umoja wa Ulaya ya Copernicus .
Ripoti hiyo ya Wanasayansi wa umoja wa Ulaya imeeleza kuwa, mwaka 2023 ulikuwa mwaka wenye joto kali zaidi kuwahi kutokea,ambapo imeripotiwa kuwa hali ya hewa imekuwa zaidi ya nyuzi joto 1.47 (Fahrenheit 2.63) ambacho ni kiwango cha juu zaidi kabla ya Mapinduzi ya viwanda.
Ripoti imesisitiza kuwa kila mwezi tangu Juni kumekuwa na rekodi mpya ya joto kali . na Novemba ilikuwa ya pekee kwa joto , hali hiyo ikiongeza wasiwasi kwa Wanasayansi kuhusu athari za sayansi katika miaka ijayo.
Ripoti hiyo inahusisha joto kali, mchanganyiko wa El Nino na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu, huku ikisisitiza hatua za haraka kwa nchi kuondoa nishati ya mafuta ili kupunguza hatari zinazoongezeka za hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.