0:00
MICHEZO
Mchezo wa Ligi kuu ya Uhispania (LALIGA) kati ya wenyeji Granada na Athletic Bilbao umelazimika kuhairishwa kufuatia kifo cha shabiki wa Granada kwenye uwanja wa Nuevo Los Cármenes.
Athletic Bilbao walitangulia kupata bao kupitia Inaki Williams, kabla ya mchezo huo kusimamishwa baada ya takribani dakika 15 pale mwamuzi alipopewa taarifa kuhusu tukio hilo jukwaani.
Wakati shabiki huyo akiendelea kupatiwa matibabu wachezaji walitolewa uwanjani na baadaye bodi ya LaLiga ilithibitisha kutokea kwa kifo cha shabiki huyo na mechi kupangwa kurudiwa tena.
Taarifa ya klabu ya Athletic Bilbao imesema
“LaLiga na vilabu vyote viwili vimekubaliana kusitisha mchezo kutokana na kifo cha shabiki huyo kwenye dimba la Los Cármenes.
Klabu ya Athletic Bilbao inatoa rambirambi zake zote . Mawazo yetu yote yako pamoja na familia ya mtu huyo na wapendwa wake”.
Related Posts 📫
HONG KONG, 🇭🇰 -
Aymeric Laporte scored with nine minutes...
PARIS, -
French billionaire and LVMH(LVMH.PA), opens new tab chairman...
MICHEZO
Beki wa klabu ya AS Roma, Evan Ndicka raia...
Consider implementing the following strategies if you want to make...